Here is the lyrics for “Lava Lava – Atajibeba ft. Platform” which was just released few days ago.
Listen and sing along.
Lava Lava – Atajibeba ft. Platform (Lyrics)
VERSE
Eti mi na yeye ndo basi tena
Eti akiniona kichefuchefu
Eeh ety hanipendi tena aah
Akiniona ata tapika
Mbona kila kwenye mbili
Nilimfanya yeye wa kwanza
Wala sikufikili angenigeuza pakacha (Pakacha)
Ooh sina lile wala hili ety mara paa! (Kaniacha)
Licha ya mabaya yake na kuyafanya yangu
BRIDGE
Ooh basi mwambieni
Kisicho riziki, ooh leo chalika ng’ari ng’ari
Alikiona cha nini
Utakipata lini, leo chalika ng’ari ng’ari
Heee! Sa mwache ajibebe
CHORUS
Atajibeba aah, atajibe atajibeba
Atajibeba atajibe
Hata aweke vigenge
Atajibeba aah atajibe atajibeba
Atajibeba atajibe
VERSE
Na kama penzi maua aah
Lilichanua kwake likasinyaa
Na kama angelijua aah
Nilivyo jitoa juu yake asingeniacha mataa
Heeeh alinikatili kwa penzi la kuigiza
Na tabasamu usoni kumbe uozo ndani viza
Sijui nazi alibadili ama alininyunyiza
Nilikua sisikii sioni bora nimempata mwingine
BRIDGE
Vijembe mama vijembe (Tara tara)
Ananipiga vijembe (Tara tara)
Kuona nalishwa peremende (Tara tara)
Wali kwa juisi ya tende ona sasa
Vijembe mama vijembe (Tara tara)
Ananipiga vijembe (Tara tara)
Ye si ndio aliniumiza (Tara tara)
Sa simtaki mwache akwe nde atajibeba
CHORUS
Atajibeba “oooh ooh” atajibe
Atajibeba, atajibeba “Acha aweke vikao” atajibe
Atajibeba atajibe (Atajibeba)
Atajibeba
OUTRO
Limemshuka shu, mmemuona
Haunitishi tishi “enhee” haunibabaishi
Haunitishi tishi, haunibabaishi
Kwa ivyo vijipost vyako
Haunitishi tishi “enhee” haunibabaishi (Pole wee)
Haunitishi tishi haunibabaishi
Vikapsheni na vifilter vyako
Haunitishi tishi “enhee” haunibabaishi (Poleee)
Haunitishi tishi haunibabaishi
Leave a Reply